27/04/2016

Belle 9 kuja na ‘remix’

28a8171C9291.jpeg
Abednego Damian ‘Belle 9’
Stori: Mayasa Mariwata
STAA wa Bongo Fleva, Abednego Damian ‘Belle 9’ hivi karibuni anatarajia kuachia ‘remix’ ya wimbo wake unaotamba kwa sasa kwenye gemu uitwao Burger Movie Selfie huku akisema utasheheni mastaa wengi wa muziki waliokubali kumpa ‘sapoti’.
Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Belle 9 alisema kwa kipindi kirefu tangu ajikite kwenye ulimwengu wa muziki katika ngoma zake zote alizowahi kuzitoa hakuna yenye sifa ya kuirudia licha ya mashabikia kumlilia kufanya hivyo, ila hii ameamua kuirudia kwa kuwa inastahili.
“Unajua wimbo wangu unafanya vizuri sana kwa sasa kwenye gemu ni wimbo ambao bado watu wanapenda kuendelea kuusikiliza kwa hiyo ili kuuboresha nimeamua kuufanyia remix nitakayoiachia hivi karibuni kwa kuwashirikisha baadhi ya mastaa ambao siko tayari kuwataja majina yao kwa sasa,” alisema Belle 9.

Angalia video na alichokiandika Diamond kuhusu kifo cha Papa Wemba





A video posted by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on
Miongoni mwa mastaa wa muziki walioguswa na kifo cha mwanamuziki nguli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Papa Wemba ni Diamond Platnumz ambaye kupitia akaunti yake ya Instagram leo ametupia video inayomuonyesha akiwa na marehemu studio huko Paris nchini Ufaransa hivi karibuni.
Papa Wemba alifariki jana baada ya kuanguka akiwa stejini huko Abidjan nchini Ivory Coast alipokuwa akifanya onyesho.

Diamond kupitia Instagram ameandika hivi; “Wiki nne tu zilizopita tulikuwa Paris, akanishirikisha kwenye nyimbo yake, tukapanga mengi juu ya wimbo halafu ghafla nasikia habari ya msiba… Dah! nimesikitika sana, hakika binadamu ni wazungumzaji tu ila Mwenyezi Mungu ndiyo mpangaji…Pumzika salama, kiongozi wetu daima tutakukumbuka🙏 #RipPapaWemba”.

26/04/2016

Pichaz: Check uzinduzi wa ‘Chura’ ulivyotia fora Maisha

UZINDUZI WA CHURA (1)
Mwanamuziki Snura Mushi akifapomu ngoma yake mpya ya Chura wakati wa uzinduzi wa video hiyo usiku wa kuamkia jana ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement, Kijitonyama jijini Dar.
UZINDUZI WA CHURA (2)
UZINDUZI WA CHURA (3)
Snura na madansa wake wakimwaga ‘nyuki’ ndani ya Maisha Basement wakati wa uzinduzi wa video ya Chura.
UZINDUZI WA CHURA (4)
Uzinduzi wa Chura ukiwa umepamba moto.
UZINDUZI WA CHURA (5) UZINDUZI WA CHURA (6)
Mashabiki wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa Chura.
UZINDUZI WA CHURA (7) UZINDUZI WA CHURA (8) UZINDUZI WA CHURA (9) UZINDUZI WA CHURA (10) UZINDUZI WA CHURA (11) UZINDUZI WA CHURA (12) UZINDUZI WA CHURA (13) UZINDUZI WA CHURA (14)
Wanenguaji wa Snura wakionyesha vimbwanga vyao wakati wa uzinduzi wa Chura.

Young D awachefua mashabiki ...........

young-dee1David Genzi ‘Young D’
Mkali wa Muziki wa Hip Hop, David Genzi ‘Young D’ amezua kioja cha aina yake baada ya kuitwa jukwaani kuimba na kuanza kuleta pozi bila sababu za msingi, jambo lililowakera mashabiki.
Tukio hilo lilijiri katika Ukumbi wa Maisha Basement, Kijitonyama, Dar ambapo bwana mdogo huyo alipoitwa  jukwaani, aligoma na kuendelea kupiga tungi kwa takriban dakika ishirini.
Baada ya kubembelezwa sana alikubali kupanda jukwaani lakini kwa dakika chache.
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, DOWNLOAD NA INSTALL APP HII ILIYOPO KWENYE PLAY STORE YAKO==>VODACOM M-PAPER APP

*********

Dida Apora Mume wa Mtu!




 CIMG0110

 Mtangazaji maarufu ambaye anafanya kazi Kituo cha Redio cha Times FM cha jijini Dar, 
                                                   Khadija Shaibu ‘Dida’

Na Gladness Mallya na Hamida Hassan, AMANI
BAGAMOYO: Mtangazaji maarufu ambaye anafanya kazi Kituo cha Redio cha Times FM cha jijini Dar es Salaam, Khadija Shaibu ‘Dida’ (pichani) anadaiwa kupora mume wa Halima Shaban, aliyeishi naye katika ndoa kwa miaka 15 na kujaaliwa watoto wawili.
  • Chanzo kinasemaje?
  • Kumbe mwanaume huyo, Issa Seleman, anatajwa pia kuwa ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ukuni, uliopo wilayani Bagamoyo, Pwani kwa miaka kumi.
mume didaMwanaume anayedaiwa kupara Dida, Issa Seleman.
  • Wakazi wa Mtaa wa Ukuni, walalamika mwenyekiti wao kutoonekana baada ya kuzama kwenye mahaba na Dida.
  • Mwenyekiti huyo ahamia Dar.
wajumbeViongozi wa Mtaa wa Ukuni
  • Dida anasemaje
  • Afunguka mengi kuhusu kuchukua mume wa mtu, adai kuwa ataolewa wakati wowote.
  • Amfungukia mwanaume huyo kutokuingia ofisini.
  • Mwanaume anasemaje?
  • Issa afunguka mengi ya moyoni kuhusu uhusiano wake na Dida.
KUFAHAMU YOTE HAYA NA MENGINE, NUNUA GAZETI LA AMANI, LEO April 21, 2016
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

Wastara Atolewa Mahari Sh. mil.5




 wastara1





Na Imelda Mtema
DAR ES SALAAM: Bahati! Siku chache baada ya nyota wa sinema za Bongo, Wastara Juma kuripotiwa kumwagwa na aliyekuwa mume wake, Sadifa Juma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge kwa Chama Cha Mapinduzi, kuna habari kuwa, mtalikiwa huyo ametolewa mahari kiasi kikitajwa kuwa ni shilingi milioni 5.
  • AMANI LAMSAKA MUOAJI
  • Bwana mdogo Juma Mbega ambaye ni mcheza filamu na mfanyabiashara wa jijini Dar, anataka kumuoa Wastara baada ya kumuona anateseka tangu kifo cha aliyekuwa mume wake, Sajuki.
  • Akili kutoa mahali ya mil 5
  • Aahidi kutuliza maumivu yote ya Wastara yaliyomtesa tangu kifo cha Sajuki.
  • Ajinadi kuitumia vyema nafasi ya aliyoiacha mbunge wa Zanzibar (Juma Sadifa).
  • WASTARA SASA
  • Afunguka ya moyoni.
  • Akili kumfahamu Juma.
  • Anena kuwa hawezi kurudisha hata senti tano kwa Sadifa.
  • Asema ana uwezo wa kuolewa hata mara kumi.
  • Sheria za Kiislam zinasemaje?
  • Kwa nini aolewe na Juma?
  • Historia ya Maisha yake ya ndoa je?
KUFAHAMU YOTE HAYA NA MENGINE, NUNUA GAZETI LA AMANI, LEO April 21, 2016
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP