29/03/2016

Fahamu tatizo la mzio au allergy-2 Dalili za mzio (allegy)

3-main-types-of-allergy
Wiki iliyopita tulieleza matatizo ya mzio na watu wanapataje lakini hatukueleza dalili zake.
Leo tunaeleza dalili za aleji ambazo ni nyingi kwa kutegemea eneo husika la mwili, lakini kwa ujumla kama ni mfumo wa hewa ndiyo ulioguswa, mtu anaweza kuwa na matatizo katika kupumua yaani akapata kikohozi au kubanwa na pumzi, makamasi na kuziba kwa pua, muwasho kwenye pua na koo, au kupumua kwa kutoa sauti kama mtu anayepiga filimbi.
allergies-texasLakini kama macho yataguswa, muhusika huhisi hali ya macho kuchoma, kutiririkwa na machozi na muwasho kwenye macho, macho kuvimba na kuwa mekundu na kadhalika.
Iwapo mtu atakula kitu ambacho ana aleji nacho anaweza kuwa na dalili kama vile kuharisha, kichefuchefu, kutapika, kusokotwa au kuumwa na tumbo na hata hali mbaya ya kutishia maisha.
Vinavyosababisha mzio au allergens vinapogusa ngozi vinaweza kusababisha ngozi kuwa na mabakamabaka, kubabuka, kuvimba, muwasho, kuota vipele na malengelenge, michubuko au ngozi kuwa nyekundu.
Aleji zinazohusisha mwili mzima zinaweza kuwa na mkusanyiko wa dalili zote tulizozitaja.
Wakati mwingine aleji inaweza kushadidisha hali ya baadhi ya watu wenye magonjwa kama ugonjwa wa ngozi wa eczema au pumu na kufanya hali iwe mbaya zaidi.
Makala yetu haya yataendelea toleo lijalo.

U.T.I; gonjwa linalosumbua wanawake

utiTIBA YA U.T.I NA USHAURI
Baada ya kuuchambua ugonjwa wa U.T. I (Urinary Tract Infection ) leo tunazungumzia tiba yake. Maambukizi katika njia ya mkojo hutibika kwa dawa mbalimbali za kisasa baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa mgonjwa ana maambukizi hayo.
Dawa ambazo anaweza kupewa mgonjwa ni kama vile Ciprofloxacin, Monurol, Furadantin, Sulfam Ethoxazole, Co-trimax, Ampicillin, Gentamicin na kadhalika. Mgonjwa anayesumbuliwa na U.T.I hapaswi kutumia dawa yoyote bila kwanza kupata ushauri wa daktari.
Wanawake wanashauriwa kuepuka kujisafisha sehemu za siri na maji machafu na yasiyo salama, pia kuepuka kupaka marashi sehemu hizo, ama kutumia pamba zenye kemikali ya kukata harufu kwani hizo huua bakteria wa asili wa sehemu za siri hali ambayo hukaribisha bakteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi.
Pia wanashauriwa wanapojisafisha baada ya kujisaidia kuanzia mbele kwenda nyuma ili kuepusha kuhamisha bakteria walio eneo la haja kubwa na kuingia njia ya mkojo.
Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauriana na daktari juu ya kutumia Oestrogen ya ukeni ili kuwasaidia kujikinga na maambukizi ya U.T.I.
Kwa mwanaume maambukizi haya huathiri nguvu za kiume na kujipenyeza hadi katika korodani na huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na kunaweza hata kusababisha ugumba. Hivyo wanashauriwa kuhakikisha wanatibu bila kuchelewa ugonjwa huo.
Pia maambukizi ya njia ya mkojo huweza kusababisha matatizo ya tezi ya kiume (prostate) kwani husababisha mrija wa mkojo kuziba, kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bakteria kujenga makazi.
Hali hiyo ikitokea mgonjwa lazima akamuone daktari ili awekewe mrija wa kutolea mkojo.
Tunaweza kuudhibiti au kuponya ugonjwa huu kwa kunywa maji mengi pamoja na juisi itokanayo na matunda halisi, iwapo tutawahi kabla tatizo halijawa sugu. Kwa maana nyingine, unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku.
Ukinywa maji ya kutosha yatakufanya uende haja ndogo kila mara na kwa njia hiyo wale bakteria watakuwa wakitoka na hatimaye kuisha kabisa.
Hivyo basi ukijisikia unaumwa tumbo chini ya kitovu, joto au maumivu wakati wa kukojoa mkojo kuwa na rangi ya njano kupindukia na kuwa na harufu kali, kutokwa na usaha wakati wa kukojoa, kabla au baada ya kukojoa, kutokwa na majimaji katika njia ya mkojo wakati wa kujisaidia haja kubwa,vichomi katika njia ya mkojo, au kuhisi kuwashwa sehemu hiyo, kuumwa kiuno, homa kali na kadhalika, nenda kamuone daktari.

yafahamu mambo 6 kuhusu yemi alade

Yemi-Alade-
Yemi Alade
Machi 13, 1989 katika Jimbo la Abia nchini Nigeria alizaliwa staa wa muziki anayewakilisha Afrika kwa sasa, Yemi Eberechi Alade.
Miaka 16 baadaye, Yemi aliingia rasmi kwenye muziki ambapo alipofikisha miaka 20 tu alibuka kidedea katika shindano la kuibua vipaji vya kuimba lililojulikana kama Peak Talent Show.
Yemi hakukata tamaa, akiwa miaka 25, Tanzania ilimuona ambapo Agosti 8, ilikuwa historia kwake kukanyaga ardhi ya JPM na kufanya bonge moja la shoo katika Tamasha la Matumaini lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar kipindi hicho akibamba na Ngoma ya Johnny.
Leo hii, Yemi ni mmoja kati ya wanamuziki wa kike wenye nguvu zaidi barani Afrika kupitia muziki.
Katika makala haya yapo mambo 6 usiyoyajua kuhusu yeye;
1. Tangu aanze muziki, hadi sasa ana albamu mbili tu, ya kwanza inayoitwa King of Queens aliyoitoa mwaka 2014 na Mama Africa aliyoitoa wiki iliyopita.
2. Yemi ana mchanganyiko wa makabila mawili maarufu nchini Nigeria. Baba ni M-yoruba na mama ni M-igbo. Jina lake la katikati anaitwa Eberechi likimaanisha Mungu Mwenye Rehema.
3. Yemi havuti sigara lakini ni mnywaji wa pombe kali. Mara nyingi hutumia kilevi pale anapokosa usingizi.
4. Video ya Johnny imemfanya kuwa mwanamuziki wa kike na wa pekee nchini Nigeria kutazamwa na watu wengi (imetizamwa zaidi ya milioni 40 katika mtandao wa Youtube).
5. Anamiliki ‘application’ katika simu za kisasa za mkononi (smart phone)ambayo inaitwa Yemi Alade. Application hiyo imemfanya kuweka rekodi ya mwanamuziki pekee nchini Nigeria kumiliki.
6. Hadi sasa ana tuzo za saba na mbili za kimataifa ambazo ni kutoka MTV Africa Music (MAMA) na Black Entertainment Television (BET).

Linah:jajuta kumtambulisha mpenzi wangu...

LinahwSTAA wa Muziki wa Kizazi Kipya, Estelina Sanga ‘Ndege Mnana’ amefunguka ya moyoni kuwa, kamwe hawezi kurudia kosa la kumuanika mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii au kwa watu na kukiri kuwa ndiyo sababu kubwa iliyochangia kuachana na mpenzi wake, William Bugeme.
Akizungumza na Showbiz kwa hisia kali msanii huyo anayebamba na Ngoma ya No Stress alisema, hakuwa akijua kama kuanika uhusiano wake kwenye mitandao ya kijamii kutamletea majanga.
“Mimi tena kumuonesha mpenzi wangu nimekoma, najutaaa! Maana kwanza wakimjua wengine watajipendekeza na kumchukua na wengine watampelekea maneno ili tugombane  hivyo bora nikae kimya labda wamjue siku ya harusi tu nimejifunza,” alisema Linah.

Ishu ya madawa ya kuulevya,Tunda amkingai kifua young D

TUNDA43David Genzi ‘Young D’ akiwa na mpenzi wake Tunda.
MUUZA nyago kwenye video za Bongo Fleva, Tunda Sebastian amejikuta akimkingia kifua mwandani wake, David Genzi ‘Young D’ kutokana na kuhusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya na kudai maneno hayo ni uzushi mtupu.
Akibonga na Showbiz alisema kuwa, anawashangaa watu ambao kila kukicha wamekuwa wakimsakama kipendacho roho wake huyo kuwa ni mtumiaji mzuri wa unga, wakati yeye ndiyo anayemjua vizuri.
“Watu wanapenda sana kuzusha yasiyofaa, sasa kama mimi ndiyo mpenzi wake na sijawahi kumuona kabisa akitumia unga wala kumuhisi hivyo iweje watu wasiomfahamu kiundani wamkomalie hilo suala, hakuna kitu kama hicho, jinsi watu wanavyomfikiria ni tofauti na alivyo,” alisema.

28/03/2016

Tangaza kipaji na biashara zako nasi..**BURE**

kama wewe unakipaji mfano: kuandika story,mashaili n.k     au una biashara au unauza au unataka kununua
kitu chochote...

         wasiliana nasi kwa ;-
                                     simu:- +255743658560
                                      email: edwinfweny00@gmail.com

Nasi tutakutangazia bira malipo yoyote.....

16-0 TFF wafungia matokeo

SIMBA-NA-STAND-8Wachezaji wa Stand United
Ibrahim Mussa, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeshtushwa na matokeo ya mchezo wa kupata bingwa wa Mkoa wa Katavi baada ya timu ya Stand FC kuibuka na ushindi wa mabao 16-0 dhidi ya Kamazima hali ambayo TFF imekiagiza Chama cha Soka Mkoa wa Katavi (KRFA) kufanya uchunguzi wa matokeo hayo.
Mchezo huo uliopigwa juzi Jumamosi, ulikuwa ni wa kumpata bingwa atakayeuwakilisha mkoa huo kwenye Ligi ya Mabingwa Mkoa ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Kabla ya mchezo huo wa mwisho, timu ya Nyundo FC ilikuwa inaongoza kwa kuwa na pointi 21 na mabao 24 ya kufunga, ambapo Stand FC ilikuwa ikihitaji ushindi wa mabao 13-0 ili kuweza kuwa bingwa wa mkoa huo.
Taarifa iliyotumwa jana na TFF, imesema: “Baada ya Stand kushinda kwa mabao 16-0, inaonyesha kuna dalili za upangaji wa matokeo, hivyo KRFA haitaruhusiwa kutangaza bingwa wa mkoa huo hadi uchunguzi utakapokamilika na TFF ijiridhishe na uchunguzi huo.”
Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni TFF ilizuia kuitangaza timu iliyopanda daraja kutoka Kundi C la Ligi Daraja la Kwanza kutokana na kuhisi kuwepo kwa vitendo kama hivyo ambapo katika mechi za mwisho, Geita Gold Sport iliifunga JKT Kanembwa mabao 8-0, huku Polisi Tabora ikiinyuka JKT Oljoro mabao 7-0.
Rihannah
2
mshindi wa fanana na Rihhana “Juliety paulo” akiwa katika pozi
3
mshindi wa fanana na Rihhana “Juliety paulo” akiwa katika pozi
20160326022439
Juliety Paulo akikabidhiwa zawadi (kushoto) na meneja wa Merry Light,Stella Daudi?(kulia)

Harmonize:ni kweli zari kaniunganisha na huddah!

harmonize kasuku - bekaboy
Staa wa Bongo fleva Rajab Abdulhan ‘Harmonize’.
Musa Mateja
Siri nje! Staa kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) anayejipenyeza kwa kasi kwenye Bongo Fleva, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ amekiri kuwa shemeji yake kwa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz;, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’,ndiye aliyemuunganisha na demu mkali kutoka Nairobi nchini Kenya, Huddah Monroe ‘The Boss Chick’.
vlcsnap-2015-11-30-16h52m54s213‘Harmonize’ akiwa na Huda.
Akizungumza ndani ya Makao Makuu ya ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge jijini Dar, wikiendi iliyopita, Harmonize alisema kuwa kwenye maisha yake hakuwahi kuwa na ndoto ya kukutana laivu na Huddah lakini bahati hiyo aliipata akiwa nchini Afrika Kusini baada ya kukutanishwa naye na Zari.
“Katika maisha yangu nilikuwa namuona tu Huddah na kumtamani ila namshukuru shemeji yangu Zari aliyenikutanisha na Huddah na kutuunganisha kuwa marafiki ambao tumekuwa tukiwasiliana utadhani tulifahamiana zaidi ya miaka hata mitano huko nyuma,” alisema Harmonize akihojiwa na Global TV Online.

shangwe za pasaka ndani ya dar live

Dar Live Pasaka (1) Dar Live Pasaka (2) Dar Live Pasaka (3) Dar Live Pasaka (4) Dar Live Pasaka (5) Dar Live Pasaka (6) Dar Live Pasaka (7) Dar Live Pasaka (8) Dar Live Pasaka (9) Dar Live Pasaka (10) Dar Live Pasaka (11) Dar Live Pasaka (12) Dar Live Pasaka (13)
Dar Live Pasaka (1) Dar Live Pasaka (2) Dar Live Pasaka (3) Dar Live Pasaka (4) Dar Live Pasaka (5) Dar Live Pasaka (6) Dar Live Pasaka (7) Dar Live Pasaka (8) Dar Live Pasaka (9) Dar Live Pasaka (10)
Dar Live (1) Dar Live (2) Dar Live (3) Dar Live (4) Dar Live (5) Dar Live (6)

penny azimia ndani ya gari..

peni3
Muonekano wa gari hilo baada ya kugongwa.
Stori:  Imelda Mtema, Wikienda
Dar es Salaam: Bidada yamemkuta! Mtangazaji wa Zuku TV, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ amekumbwa na mkasa mwingine baada ya gari lake kupigwa mzinga maeneo ya Mikocheni jijini Dar, kwa kile kinachodaiwa alizimia barabarani kutokana na tatizo la ini linalomsumbua kwa sasa.
Chanzo makini ambacho kilishuhudia tukio hilo kilisema kuwa staa huyo alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota Mark X kwa mwendo wa kawaida lakini akaanza kupunguza spidi taratatibu kutokana na maumivu yaliyompata ghafla na kusababisha bodaboda kugonga gari lake kwa nyuma.
peni2Mashuhuda wakiwa kwenye tukio.
Mpashaji wetu aliendelea kusema kuwa, wakati tukio hilo linatokea ilikuwa mchana kweupe bodaboda nusura wamfanyizie.
Pamoja na watu kusogelea kwenye tukio, Penny aliendelea kukaa ndani ya gari akiwa amejilaza hadi alipopata nafuu ndipo akaanza kuondoa gari taratibu.
Wikienda lilipozungumza na Penny alisema alipatwa na hali hiyo huku mwili ukiishiwa nguvu lakini kwa sasa yuko sawa.
pennyMtangazaji wa Zuku TV, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’.
Penny anakabiliwa na tatizo la kuharibika kwa ini kufuatia unywaji wa pombe kali kwa muda mrefu.
Hivi karibuni, Penny aliyekuwa mpenzi wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aliripotiwa kuwa na tatizo la ini kutokana na unywaji wa pombe kali.

wastara atoroshwa hospitalini...

DSC_5306Staa wa Bongo Muvi, Wastara Juma akiwa hoi hospitali.
Stori:   Dustan Shekidele, Wikienda
Morogoro: Taarifa mbaya! Staa wa Bongo Muvi, Wastara Juma ambaye mapema wiki iliyopita alidai kupewa talaka la mumewe, Sadifa Khamis Juma, Mbunge wa Donge, Zanzibar, anadaiwa kutoroshwa hospitalini kisha kupelekwa hoteli ya mafichoni huku akiendelea na matibabu.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara aliyekuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Misheni ya St. Herry Health Center iliyopo mjini hapa, aliondolewa wodini hapa usiku mnene huku akiwa bado hali yake ya kiafya haijatengamaa tangu alipolazwa mapema wiki iliyopita akisumbuliwa na presha na kisukari na baadaye kupoteza fahamu.DSC_5305
Nesi akimuhudumia.
Wikienda lilifika hospitalini hapo Jumamosi iliyopita na kuthibitishiwa kuondolewa kwa msanii huyo na mtu aliyedai kuwa ni babu yake aliyetajwa kwa jina la Abdulaziz Babu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wahudumu waliokuwa zamu walioomba hifadhi ya majina, jamaa huyo alidai kuwa Wastara aruhusiwe kwani alihofia usalama wake na kwamba sehemu aliyopanga kumpeleka ni salama zaidi.
Baada ya kunusa ‘ubuyu’ huo hospitalini hapo, Wikienda lilimsaka Wastara kujua mahali alipo na hali yake lakini jitihada hizo ziligonga mwamba kwa kuwa namba yake ya simu haikuwa hewani.
DSC_5304Alipotafutwa mtu huyo anayedai ni babu wa Wastara alifunguka: “Ni kweli nimemuondoa Wastara hapo hospitalini kwa sababu za kiusalama. Yupo hotelini lakini siwezi kukuelekeza ni sehemu gani kwa sababu ukiandika itajulikana na tatizo litakuwa palepale.”
Wastara alikumbwa na hali hiyo ikidaiwa ilitokana na mgogoro wa ndoa yake na Sadifa iliyofungwa hivi karibuni na kushindwa kudumu.

19/03/2016

Diamond avunja record marekani,ukumbi umefurika na mamia ya watu washindwa kuingia ndani.....


Ni show ambayo ilifanyika Las Vegas Marekani ambapo Promota DMK akisaidiana na wenzake waliandaa kuwapa burudani Waafrika mbalimbali kwenye mji huo March 2016                                            






angalia hapa; https://www.youtube.com/watch?v=YbQWlD8ZUbU




https://www.youtube.com/watch?v=YbQWlD8ZUbU

17/03/2016

mama diamond atoa siri

   











Mama Diamond Platnumz, Sanura Kassim ‘Sandra’
Stori:  Musa Mateja, Wikienda
Dar es Salaam: Mama mzazi wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ametoboa siri ya mkaza mwanaye, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kushindwa kuishi Bongo na badala yake kukimbilia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Sandra au Mama D aliyasema hayo katika mahojiano maalum na Ijumaa Wikienda juu ya uhusiano wake na Zari kufuatia tetesi kuwa hawaivi ndipo akaweka mambo sawa.

Mama D alisema kuwa yeye na Zari wapo vizuri lakini kinachomfanya mkwewe huyo kushindwa kuishi naye Bongo ni kutokana na biashara zake kudoda nchini Afrika Kusini.
“Unajua anapokuwa huku (Bongo), biashara zake huwa zinayumba sana, wakati mwingine akipiga simu akiulizia biashara zinakwendaje anaambiwa hali ni mbaya au hazijaingiza chochote hapo ndipo huwa anachanganyikiwa.
ZarimondDiamond na mpenzi wake, Zari.
“Kwa mfano hivi karibuni alipiga simu akaambiwa hakuna fedha kabisa na biashara haziendi. Kilichofuata ni kujiandaa na kumchukua Tiffah (Latifah Nasibu) kisha akaondoka zake.
“Hicho ndicho kinachomkimbiza Zari kuishi Bongo na si kweli kwamba hapapendi au kuna tatizo lolote,” alisema Mama D.