Mama Diamond Platnumz, Sanura Kassim ‘Sandra’
Stori: Musa Mateja, Wikienda
Dar es Salaam: Mama mzazi wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ametoboa siri ya mkaza mwanaye, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kushindwa kuishi Bongo na badala yake kukimbilia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

Sandra au Mama D aliyasema hayo katika
mahojiano maalum na Ijumaa Wikienda juu ya uhusiano wake na Zari
kufuatia tetesi kuwa hawaivi ndipo akaweka mambo sawa.
Mama D alisema kuwa yeye na Zari wapo
vizuri lakini kinachomfanya mkwewe huyo kushindwa kuishi naye Bongo ni
kutokana na biashara zake kudoda nchini Afrika Kusini.
“Unajua anapokuwa huku (Bongo), biashara
zake huwa zinayumba sana, wakati mwingine akipiga simu akiulizia
biashara zinakwendaje anaambiwa hali ni mbaya au hazijaingiza chochote
hapo ndipo huwa anachanganyikiwa.
“Kwa mfano hivi karibuni alipiga simu
akaambiwa hakuna fedha kabisa na biashara haziendi. Kilichofuata ni
kujiandaa na kumchukua Tiffah (Latifah Nasibu) kisha akaondoka zake.
“Hicho ndicho kinachomkimbiza Zari kuishi Bongo na si kweli kwamba hapapendi au kuna tatizo lolote,” alisema Mama D.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni