14/09/2016

Zari adaiwa kutishia kutoa mimba!

Zari adaiwa kutishia kutoa mimba!

zari (1) Zarinah Hassan ‘Zari’
Stori:  Musa Mateja, Ijumaa
DAR ES SALAAM Hakuna ubishi kuwa mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ ni mjamzito lakini habari ambayo hujaisikia ni kwamba hivi karibuni mwanamama huyo alidaiwa kutaka kuichoropoa mimba hiyo.
lynnKisa Lynn
Chanzo chetu ambacho ni rafiki wa karibu wa Diamond kilitumwagia ubuyu kuwa, baada ya yale madai kuwa Diamond anatoka na yule Video Queen wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Irene Hilary ’Lynn’, Zari alimaindi kinoma na kufikia hatua ya kutaka kuitoa mimba ili kumkomoa Diamond.
Inadaiwa kuwa, kilichomkasirisha zaidi Zari ni kitendo cha mama wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kuonesha kufurahia kitendo cha mwanaye kumsaliti.
ZarimondDiamond na Zari
“Ninyi hamjui tu jinsi ile skendo ya Diamond kutoka na Lynn ilivyotaka kuleta balaa, unaambiwa Zari alitishia kutoa mimba, mbaya zaidi ni pale zilipoibuka tena taarifa kuwa, Lynn ana mimba, mbona ulikuwa mtiti?” kilidai chanzo hicho.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa, kutokana na hali hiyo, Diamond alitumia nguvu kubwa kumsihi mzazi mwenzake huyo kutosikiliza maneno ya watu na badala yake aitunze mimba hiyo ili amzalie mtoto wa pili baada ya Tiffah ambaye sasa ana umri wa mwaka mmoja.
zari (2)Madai hayo yalimfanya paparazi wetu amtafute Diamond ‘Baba Tiffah’ kwa njia ya simu kuyazungumzia ambapo alipopatikana alisema: “Unajua uhusiano una changamoto nyingi sana lakini ninachoweza kushukuru ni kwamba leo hii mimba ya baby wangu ina zaidi ya miezi minne na Mungu akijaalia mwezi Desemba nitapata mtoto mwingine wa kiume, hayo mengine tuyaache.”
Akaongeza: “Unajua watu wanaongea sana hasa kwenye mitandao ya kijamii lakini sisi ni waelewa na hatuwezi kuwapa watu nafasi watuharibie.”
Diamond na Zari wamekuwa kwenye uhusiano wenye figisu nyingi huku wengine wakidai hawawezi kudumu kutokana na msanii huyo kudaiwa mara kadhaa kusaliti ambapo skendo mbichi inayomtafuna ni ya kuwapachika mimba Lynn na modo Hamisa Mobeto.
Tupia Comment Yako Hapa

Shilole; kilichokupata feri ni sawa tu, kwa nini ulalamike?

Shilole; kilichokupata feri ni sawa tu, kwa nini ulalamike?

shilole n tatooZUWENA Mohammed ndilo jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa nyumbani kwao Igunga, mji mdogo, lakini maarufu mkoani Tabora. Lakini katika harakati za maisha, amejikuta akipata umaarufu mkubwa nchi nzima na jirani, kwa jina lake la kisanii la Shilole.
Wengine wanamuita Shishi Baby. Huyu anathibitisha kuwa mwanamke akiamua, inawezekana. Kwa sababu historia yake inaonesha kuwa ni mpambanaji, akitokea kudhalilishwa kimapenzi akiwa na umri mdogo, hadi kuja kuwa staa mkubwa.
Katika muziki, anafanya vizuri sana, kwani kila kukicha, anaonesha kuendelea, akifanya aina ya muziki ambao awali ulikuwa Mduara, lakini kwa sasa ameuongeza vionjo vinavyomfanya kuwa kivutio cha aina yake stejini.
Ana kazi nyingi nzuri, tangu alipoanza na wimbo wake wa Lawama, zikiwemo Dume Dada, Paka la Bar, Chuna Buzi, Namchuka, Malele, Nyang’angany’a na sasa kibao kipya alichomshirikisha Barnaba, Say My Name.
Hata hivyo, kama ilivyo kwa binadamu wote, nje ya sanaa, ana maisha binafsi yanayoendana na matukio ambayo mengi yanachagizwa na ustaa wake. Kwa mfano juzikati, akiwa na washkaji ndani ya pantoni kuelekea Kigamboni.
Akiwa ndani ya gari na kidogo akionekana kuchangamka, alikataa kushuka garini kama utaratibu ulivyo. Gari halitakiwi kupakiwa kwenye pantoni likiwa na abiria, anatakiwa dereva tu, ili aweze kulidhibiti endapo kutatokea dharura yoyote.
Shishi Baby alikataa katakata kushuka, akiwaambia walinzi kuwa yeye ni staa mkubwa, hivyo aachwe avuke akiwa ‘amejilalia’ zake garini, jambo ambalo halikukubaliwa, hivyo kuwafanya walinzi hao kumshusha kwa nguvu na ‘kumpumzisha’ kwa muda ili kiburudisho alichopata kipunguze makali.
Hili ndilo tatizo moja kubwa sana kwa hawa mastaa wetu, hasa hawa wa dotcom. Wanaamini kujulikana kwao ndiyo leseni ya kufanya wanavyotaka, bila kujali kuwa kuna sheria na taratibu ambazo lazima zifuatwe, bila kujali ‘taito’ yako, iwe msanii, mwanasiasa, mwanasheria au yeyote yule.
Na ubaya zaidi, hawafahamu kuwa wao ndiyo wanastahili kuwa namba moja katika kuzifuata na kuzitii sheria na taratibu hizo, ili wawe mifano kwa wengine, hasa mashabiki wao.
Inashangaza kuwa hawafahamu kwamba kuna watu ukiwatajia Shilole wala hata hawaelewi unasema nini. Siyo kila mtu anafuatilia muziki, filamu au chochote unachokifanya. Sasa unapoingia kwenye kazi ya mtu na kusema eti; ‘kwani hunijui mimi?’ unampa majaribu tu ya bure. Kwani wewe nani katika nchi hii?
Unaweza kufika ofisi ya umma na kujitambulisha, ukitegemea kila mtu anakufahamu, hapana. Kuna wengine hawafuatilii kabisa Bongo Fleva, hawajui hata filamu za Kibongo zikoje, sasa wakisema hawakujui usifikiri wanatania na hata kama wanakujua, ndiyo uvunje sheria?
Nimshauri tu dada yangu Shilole, katika kufuata sheria na taratibu, anapaswa kuwa mstari wa mbele ili wanaomshabikia nao watambue kuwa wanapaswa kuzingatia, vinginevyo kama unataka kuutumia ustaa, basi ni kwenye viwanja vya burudani ambako wanaofika ni wale wanaokufahamu.

Diamond amtusi Wastara

 http://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2016/07/diamond.jpg



HAMIDA HASSAN, WIKIENDA
DAR ES SALAAM: Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anadaiwa kumtusi staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma baada ya kumuomba msanii wake akarekodie katika studio zake za Wasafi Classic Baby (WCB).
Tukio hilo lililopigwa chabo na chanzo chetu lilijiri wikiendi iliyopita katika moja ya studio za runinga ambapo Wastara alikwenda kumpeleka msanii wake aitwaye Ibrahim Khaan kwa ajili ya mahojiano.
Sosi wetu aliliambia Wikienda kuwa, Diamond alimshushia Wastara matusi kwa madai kuwa ni shabiki wa Ali Kiba na kwamba kwa muda mrefu alikuwa akimsaka ili ampe makavu.
wastara (2)Wastara Juma.
CHANZO CHAFUNGUKA
“Jamani mimi nimemsikia kwa masikio yangu Diamond akimtukana Wastara matusi
 ya nguoni, kisa ni ushabiki wake kwa Ali Kiba.
“Unajua Wastara ana msanii wake ambaye ‘anammeneji’, walipokuwa kwenye studio za runinga walikutana na meneja wa Harmonize anayeitwa Momo.
“Huyo Momo anajuana na mdogo wa Wastara hivyo walipoonana walisalimiana kisha akatokea Harmonize ambaye naye alisalimiana na Wastara.
“Wastara ndiye aliyeomba kuonana na Diamond kwa sababu msanii wake alikuwa akihitaji kubadilishana naye mawazo,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, baada ya kuongea na Wastara, Momo alimfuata Diamond kwenye gari akiwa ameongozana na mdogo wa Wastara ambaye alimweleza Diamond kuwa Wastara alikuwa akitaka kuongea naye.
Chanzo kiliendelea kusimulia kuwa Diamond, alianza kutoa maneno mazito na kusema kwa nini asiende kwa Ali Kiba kisha akatukana matusi mazito yasiyoandikika gazetini.
Chanzo hicho kilidai kwamba, wakati Diamond akitoa lugha hiyo kali kwa Wastara, Harmonize alikuwa pembeni hivyo aliinama kwa aibu.
WASTARA NA DIAMOND
Ilisemekana kuwa, Wastara alipomsogelea Diamond alimsalimia Diamond ambaye aliitikia akiwa amekasirika kisha Wastara akaanza kujieleza kuwa alikuwa akihitaji msanii wake akafanyie kazi yake kwenye Studio za Wasafi.
Chanzo kilieleza kuwa Diamond aliendelea kumkejeli Wastara akimhoji kwa nini Wasafi na si kwa Ali Kiba?
Ilielezwa kuwa Wastara alicheka na kumwambia kuwa yeye amependa kurekodia Wasafi na nia yake si ushabiki bali ni kazi tu.
DIAMOND AKATISHA MAONGEZI
Hata hivyo, ilisemekana kwamba, Diamond hakutaka maongezi hivyo alimkatisha kwa kumwambia kuwa jambo hilo amalizane na Momo.
Baada ya habari hiyo kutua kwenye dawati la Wikienda, mwanahabari wetu alimtafuta Wastara kwa njia ya simu ambapo alikiri kukutana na Diamond na kuzungumza naye ishu za msanii wake lakini hakujua kama kulikuwa na matusi.
“Sina ugomvi naye na wala hayo ya matusi sijui ila ni kweli nilikutana naye na nilipanga kwenda kwenye studio yake lakini alinihoji kuhusiana na kuichagua studio yake, nikamweleza natafuta ubora na nitafanyia studio mbalimbali ikiwa ni pamoja na huyo Ali Kiba,” alisema Wastara.
Wikienda lilimtafuta Diamond kwa njia ya simu lakini jitihada za kumpata ziligonga mwamba baada ya kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa hivyo zinaendelea.

13/09/2016

Samsung Galaxy Note7 Zapigwa Marufuku Kwenye Ndege


Samsung Galaxy Note7 Zapigwa Marufuku Kwenye Ndege



epa_samsung_note_7_ml_160902_12x5_1600Maafisa wa uchukuzi wa ndege nchini Marekani wamewatahadharisha abiria wanaosafiri kwa ndege kutofungulia au kuchaji simu za Samsung Galaxy Note 7 smartphones wakiwa ndani ya ndege.
Onyo hilo limetolewa ikiwa ni siku chache bada ya kuipotiwa kwa simu hizo kuwa zimekuwa zikiripuka aidha zikiwa zinachajiwa au mtumiaji akiwa anaongea au hata kama ikigusa sehemu yenye joto kidogo tu. Hii ni kutokana na aina za betri za simu hizoambazo zimetengenezwa kwa chaji (ions) zitokanazo na madini ya lithium (lithium-ion).
_91003684_gettyimages-588328896Taasisi ya Uchukuzi wa Ndege Marekani (FAA) pia imewashauri watu kutoweka simu hizo kwenye mizigo ambayo wanaingia nayo eneo wanamoketi abiria kwenye ndege. Taasisi hiyo imekuwa ikiendesha ukaguzi maalumkwenye mabegi ya abiria wake ili kugundua kama abiria amebeba Samsung Galaxy Note 7 au la!
Kampuni ya Samsung ilisitisha uuzaji wa simu hizo na kukubali kwamba kulikuwa na hitilafu wakati wa uundaji wa betri za simu hizo. Kampuni hiyo hata hivyo ilisema ni vigumu kutambua ni simu gani zilizo na kasoro.
_90995808_burntnotearielgonzalezMashirika ya Australia ya Qantas na Virgin Australia pia yamewashauri wateja kutoweka chaji simu zao au hata kuzitumia wanaposafiri kwa ndege.
Mbali na kasoro hizo, simu hiyo ambayo ilizinduliwa mwezi uliopita imefurahiwa na wateja ambapo simu takriban 2.5 milioni za Note 7 zilikuwa zimesafirishwa maeneo mbalimbali duniani.
Samsung wamesema wateja ambao tayari walikuwa wamenunua simu hizo, na zimepata hitilafu, watapewa fursa ya kuzibadilisha. Shughuli ya kupata simu mpya itachukua takriban wiki mbili.

Darasa: Bila mimi hakuna Mavoko

Darasa: Bila mimi hakuna Mavoko

darasaSharif Ramadhani ‘Darasa’
BONIPHACE NGUMIJE
MWANAMUZIKI wa Hip Hop Bongo anayetamba na Ngoma ya Too Much, Sharif Ramadhani ‘Darasa’ amefunguka kuwa bila yeye kumshirikisha msanii wa Bongo Fleva, Rich Mavoko kwenye ngoma yake ya Kama Utanipenda angepotea kimuziki.
mavoko (1)Rich Mavoko
Akich-onga na Showbiz Xtra, Darasa alisema kuwa Mavoko ni mkali lakini kuna wakati ulifika akaanza kama kupoteza nguvu aliyokuwa nayo kwenye gemu hivyo baada ya kumshir-ikisha kwenye wimbo wake huo amerudi kwenye reli
 jambo ambalo anajivunia.
“Sikatai kuwa Mavoko ni mkali, lakini hakuna asiyefahamu kuwa kuna wakati alianza kama kupotea hivi kwenye gemu na mimi ndiye niliyemrudisha tena baada ya kumshirikisha kwenye wimbo wangu, Kama Utanipenda!” alisema Darasa.

TRA yapiga mnada Range la Wema!

TRA yapiga mnada Range la Wema!

WEMA2Wema Sepetu
Gladness Mallya, Amani
DAR ES SALAAM: Bila huruma! Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeliingiza sokoni lile gari la kifahari aina ya Range Rover Evouge la Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kwa madai ya ukwepaji wa kodi, Amani limetonywa!
Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya TRA, Ofisi Kuu jijini Dar es Salaam (long room), Evouge la Wema liko mnadani kinachosubiriwa ni tarehe ya kuita wateja kwa ajili ya manunuzi.
gari la wemaRange Rover Evouge la Wema.
KISA CHA MNADA
“Lile gari linaonesha liliingia nchini kutoka Msumbiji ambako mtu wa kwanza alikuwa ni Mussa Anli akiwa na makao nchini humo.
“Lakini baada ya kufika kwa Wema likaonekana kutokuwa na uhalali wa kuwepo nchini, hasa kwa upande wa mapato ya nchi. Likakamatwa na mmiliki wake (Wema) alipewa siku za kulipa, hajafanikisha hilo. Kwa hiyo likawa liko nchini kinyume na utaratibu (overstayed), ndiyo maana TRA imeamua kuliuza ili fedha za mapato ziingie serikalini.”
SIKU YA MNADA
Chanzo: “Mnada utafanyika Julai 18, mwaka huu kule bandarini kwenye warehouse (ghala la kuhifadhia bidhaa). Kwa hiyo kila kitu kitakuwa pale. Itakuwa Jumapili kuanzisa saa 4 asubuhi na kuendelea.”
MASHARTI YA UNUNUZI
Chanzo: “Mtu atakeyeshida mnada, atatakiwa kulipa asilimia 25 on the spot (papohapo) halafu asimilia 75 itakayosalia lazima ilipwe ndani ya saa 48 tangu kufanyika kwa mnada.
“Lakini pia, gari litatakiwa kuondolewa eneo la mnada baada ya mnunuzi kumaliza kulipa asilimia 75 iliyobaki.”
GAZETI LA SERIKALI
Chanzo chetu kilikwenda mbele kwa kusema kuwa, TRA imefuata taratibu zote za uuzaji wa gari hilo kwani kupitia Gazeti la Serikali la Daily News la Juni 16, mwaka huu, ilitangaza mnada huo kama sheria inavyotaka.
WATEJA WATEMBELEA
Kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya wateja wameanza kutembelea eneo hilo ili kujionea gari hilo ambalo ni jipya katika matumizi.
MBALI NA GARI LA WEMA
Hata hivyo, chanzo chetu kilisema kuwa, mbali na gari la nyota huyo, bidhaa nyingine mbalimbali zitapigwa mnada kwa watu watakaopenda kununua, kama TV, magari, mafuta ya kupikia na mifuko ya sukari.
WEMA AMEFIKAJE HAPA?
Katika sherehe yake ya siku ya kuzaliwa ‘bethidei’, Novemba mwaka jana, (kawaida ni Septemba 28),  Wema alitangaza hadharani kwamba, alilinunua gari hilo kwa dola za Kimarekani 90,000 (zilikuwa si chini ya shilingi milioni 200) huku akisema ni mali yake.
ILIANDIKWA
Hata hivyo, siku chache baadaye, gazeti hilihili liliandika kwa kufuata chanzo kimoja kutoka TRA kikinyetisha kwamba, kasi ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ kuhakikisha hakuna Mtanzania anayekwepa kulipa kodi, gari hilo la kifahari linachunguzwa na mamlaka hiyo.
WASIWASI WA VIPATO
Chanzo hicho kilisema kuwa, uchunguzi wa gari hilo pamoja na mengine ya mastaa wa Bongo, ulitokana na mamlaka kuwa na wasiwasi na usahihi wa kulipa kodi kwa sababu ya maisha yao ya kifahari huku vipato vyao vikiwa haviko wazi.
ALIKAMATWA
Januari mwaka huu, Wema akiwa na gari hilo maeneo ya Aficana, Mbezi-Beach jijini Dar wakati akiwa anakwenda kwenye bethidei ya rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Kibadude, alikamatwa na watu wa TRA kwa makosa ya kuliendesha bila vibali na kubainika kuwa, lilikuwa na ‘figisufigisu’ katika uhalali wa kuingia nchini.
KIGOGO ALIMUOKOA
Hata hivyo, katika sakata hilo, kiogozi mmoja serikalini aliwaambia watu wa TRA kumpa siku saba msanii huyo kuwasilisha  nyaraka bila kuliendesha gari hilo kinyume cha siku hizo, lichukuliwe na TRA kwa ajili ya mnada jambo ambalo lilitimia na sasa gari hilo lipo manadani.
MKURUGENZI WALIPA KODI
Baada ya madai hayo, Amani lilimtafuta Mkurugenzi wa Elimu kwa Walipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo ili kumsikia anasemaje kuhusu hilo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
WEMA ASAKWA JUZI
Ili kuweka sawa mzani wa habari, juzi Jumanne, Amani lilimpigia simu Wema lakini iliita bila kupokelewa. Alipopigiwa simu mtu mmoja wa karibu yake, alisema haikuwa rahisi kwa Wema kupokea simu kwani alikuwa Uwanja wa Taifa, Dar kuangalia mpambano wa Timu ya Yanga na TP- Mazembe kutoka DRC.

MPYA : selection za vyuo (undergraduate degree) 2016/17



Tokeo la picha la TCU.GO.TZ

Kama kawaida yetu town tops katika nusanusa yetu tumefanikiwa kunasa hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa na watu wengi,ni kuhusu majina ya wanafunzi waliochaguliwa na TCU 2016/2017 kujiunga vyuo vikuu mbalimbali 2016/2017.
 wale wote mlioomba vyuo kama,

  • Chuo Kikuu cha Ardhi, (ARU)
  • Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki (HKMU),
  • International Medical and Technological University (IMTU)
  • Moshi University College of Cooperative and Business Studies(MUCOOBS-MOCCU)
  • Chuo Kikuu cha Mlima Meru
  • Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS)
  • Chuo Kikuu cha Morogoro (MUM)
  • Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU)
  • Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)
  • Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO)
  • Chuo Kikuu St. Augustine cha Tanzania (SAUT)
  • Chuo Kikuu St. John cha Tanzania (SJUT)
  • Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA)
  • Chuo Kikuu cha Zanzibar
  • Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji-TEKU
  • Chuo Kikuu cha Tumaini (TU)
  • Chuo Kikuu cha Bukoba
  • Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), established in 1970 from the split of the Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki
  • Chuo Kikuu cha Dodoma,UDOM
  • Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU)


NOTE:LINK IMEKAA POA ,ANDAA USERNAME NA PASWORD YAKO ILI UONE KAMA UMECHAGULIWA KWA KU LOGIN KWENYE PROFILE YAKO! 


 ili kujua ulipo chaguliwa,bofya hapa>>>

MPYA:HIVI NDIO VYUO VIKUU VYENYE NAFASI KWA FORM 6 WALIOKOSA KUCHAGULIWA FIRST ROUND 2016/2017

MPYA:HIVI NDIO VYUO VIKUU VYENYE NAFASI KWA FORM 6 WALIOKOSA KUCHAGULIWA FIRST ROUND 2016/2017


Image result for tcu.go.tz