Samsung Galaxy Note7 Zapigwa Marufuku Kwenye Ndege
Onyo hilo limetolewa ikiwa ni siku
chache bada ya kuipotiwa kwa simu hizo kuwa zimekuwa zikiripuka aidha
zikiwa zinachajiwa au mtumiaji akiwa anaongea au hata kama ikigusa
sehemu yenye joto kidogo tu. Hii ni kutokana na aina za betri za simu
hizoambazo zimetengenezwa kwa chaji (ions) zitokanazo na madini ya lithium (lithium-ion).
Kampuni ya Samsung ilisitisha uuzaji wa
simu hizo na kukubali kwamba kulikuwa na hitilafu wakati wa uundaji wa
betri za simu hizo. Kampuni hiyo hata hivyo ilisema ni vigumu kutambua
ni simu gani zilizo na kasoro.
Mbali na kasoro hizo, simu hiyo ambayo
ilizinduliwa mwezi uliopita imefurahiwa na wateja ambapo simu takriban
2.5 milioni za Note 7 zilikuwa zimesafirishwa maeneo mbalimbali duniani.
Samsung wamesema wateja ambao tayari
walikuwa wamenunua simu hizo, na zimepata hitilafu, watapewa fursa ya
kuzibadilisha. Shughuli ya kupata simu mpya itachukua takriban wiki
mbili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni