Darasa: Bila mimi hakuna Mavoko
BONIPHACE NGUMIJE
MWANAMUZIKI wa Hip Hop Bongo
anayetamba na Ngoma ya Too Much, Sharif Ramadhani ‘Darasa’ amefunguka
kuwa bila yeye kumshirikisha msanii wa Bongo Fleva, Rich Mavoko kwenye
ngoma yake ya Kama Utanipenda angepotea kimuziki.
Akich-onga na Showbiz Xtra, Darasa
alisema kuwa Mavoko ni mkali lakini kuna wakati ulifika akaanza kama
kupoteza nguvu aliyokuwa nayo kwenye gemu hivyo baada ya kumshir-ikisha
kwenye wimbo wake huo amerudi kwenye reli
jambo ambalo anajivunia.
“Sikatai kuwa Mavoko ni mkali, lakini
hakuna asiyefahamu kuwa kuna wakati alianza kama kupotea hivi kwenye
gemu na mimi ndiye niliyemrudisha tena baada ya kumshirikisha kwenye
wimbo wangu, Kama Utanipenda!” alisema Darasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni