Zari adaiwa kutishia kutoa mimba!
Stori: Musa Mateja, Ijumaa
DAR ES SALAAM Hakuna ubishi kuwa
mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan
‘Zari’ ni mjamzito lakini habari ambayo hujaisikia ni kwamba hivi
karibuni mwanamama huyo alidaiwa kutaka kuichoropoa mimba hiyo.
Chanzo chetu ambacho ni rafiki wa karibu
wa Diamond kilitumwagia ubuyu kuwa, baada ya yale madai kuwa Diamond
anatoka na yule Video Queen wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Irene Hilary
’Lynn’, Zari alimaindi kinoma na kufikia hatua ya kutaka kuitoa mimba
ili kumkomoa Diamond.
Inadaiwa kuwa, kilichomkasirisha zaidi
Zari ni kitendo cha mama wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kuonesha
kufurahia kitendo cha mwanaye kumsaliti.
“Ninyi hamjui tu jinsi ile skendo ya
Diamond kutoka na Lynn ilivyotaka kuleta balaa, unaambiwa Zari alitishia
kutoa mimba, mbaya zaidi ni pale zilipoibuka tena taarifa kuwa, Lynn
ana mimba, mbona ulikuwa mtiti?” kilidai chanzo hicho.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa, kutokana na
hali hiyo, Diamond alitumia nguvu kubwa kumsihi mzazi mwenzake huyo
kutosikiliza maneno ya watu na badala yake aitunze mimba hiyo ili
amzalie mtoto wa pili baada ya Tiffah ambaye sasa ana umri wa mwaka
mmoja.
Akaongeza: “Unajua watu wanaongea sana
hasa kwenye mitandao ya kijamii lakini sisi ni waelewa na hatuwezi
kuwapa watu nafasi watuharibie.”
Diamond na Zari wamekuwa kwenye uhusiano
wenye figisu nyingi huku wengine wakidai hawawezi kudumu kutokana na
msanii huyo kudaiwa mara kadhaa kusaliti ambapo skendo mbichi
inayomtafuna ni ya kuwapachika mimba Lynn na modo Hamisa Mobeto.
Tupia Comment Yako Hapa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni