Akizungumza na Showbiz kwa hisia kali
msanii huyo anayebamba na Ngoma ya No Stress alisema, hakuwa akijua kama
kuanika uhusiano wake kwenye mitandao ya kijamii kutamletea majanga.
“Mimi tena kumuonesha mpenzi wangu
nimekoma, najutaaa! Maana kwanza wakimjua wengine watajipendekeza na
kumchukua na wengine watampelekea maneno ili tugombane hivyo bora nikae
kimya labda wamjue siku ya harusi tu nimejifunza,” alisema Linah.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni