Stori: Hamida Hassan, Ijumaa
MSANII nyota wa Muziki wa Kizazi
Kipya, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole, baada ya kusemwa kwa muda
mrefu, hatimaye amefunguka na kutoa sababu nne za yeye kupenda kutoka na
wanaume wanaotajwa kuwa ni wadogo kwake kiumri.
Akizungumza na Ijumaa, nyota
huyo ambaye pia hufahamika kama Shishi Baby, alisema maneno ya watu juu
ya jambo hilo siyo sahihi, kwani historia ya maisha aliyopitia ndiyo
inayomfanya aonekane mkubwa, wakati yeye ni binti mdogo aliyezaa mapema.
Aidha, mkali huyo wa kibao cha Paka la
Baa, alisema yeye hivi sasa ana umri wa miaka 30, ‘size’ kabisa kwa
wanaume anaotoka nao kimapenzi, kwani hata hao nao, siyo watoto
‘kihiiivyo’ kama maneno ya watu yanavyosema.
Sababu nyingine ni;
1: KUOGOPA KUZEESHWA
“Mimi ni kijana kutembea na wazee
siwezi, naweza kujikuta nimezeeshwa bure kitu ambacho sikitaki hata
kukisikia, kwani naamini bado nina uhitaji kama kijana.
“Angalia wasichana wengi wadogo
wanaotoka kimapenzi na wazee hujikuta nao wanakuwa na mambo ya kizee,
unadhani atafanya nini wakati ameshakubali kuzeeshwa?”
2: HATAKI KUBURUZWA
“Mimi napenda kuchakarika ndiyo maana
sipendi kabisa penzi la wazee ambao ukiwa tegemezi kwao wanakuburuza.
Wanawake wengi wanaotoka na wazee huwategemea kwa sababu ya uvivu wao wa
kutafuta, kwangu mimi kazi tu!
3: ANASAKA PENZI LA KWELI
“Wasichana wengi wa mjini wamekuwa
wakijiingiza kwa wazee lakini hawana mapenzi nao ya kweli, wanakwenda
kuchuna pesa kisha wana viserengeti, mimi mwenzao nafuata penzi kwa hao
vijana, wanajua kupenda na kwa sababu hobi yangu ni wao siwezi kuwa na
wazee kwa kweli.”
4: VIJANA WANA NGUVU, WANAVUTIA
“Na uweke pia hii, kwamba vijana wana nguvu, damu changa na wanavutia, siwezi kutoka na wazee hawana mvuto.”
Baada ya kutaja sababu zake hizo,
Shilole alihoji ni yupi mwenye afadhali kati yake na wasichana wenzake
wanaotoka na wazee lakini wakiwa wavivu kutafuta?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni